Advertisemen
Wapiganaji wa kundi la wanamgambo la
Al shaabab walimezima shambulizi la kuvizia lililotekelezwa na
makomando wa jeshi la Marekani usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa
Afisa mmoja wa ngazi ya juu jeshini ambaye hakutaka jina lake litajwe
anasema kuwa shambulizi hilo lililotekelezwa na vikosi vya usalama la
Marekani kwa ushirikiano na majeshi ya Somalia yalifanikishwa kwa kuruka
kwa ndege za helikopta kwa kambi ya wapiganaji hao iliyoko Awdhegle,
takriban kilomita 50 Kusini mwa Somalia.Afisa huyo amethibitisha kuwa Makomando hao wa Marekani walihusika katika uvamizi huo.
Awali kundi la wanamgambo hao lilikuwa limesema kuwa lilizima shambulizi la kuvizia lililotekelezwa katika mojawepo ya kambi zao kwa njia ya helikopta.
Wenyeji wa eneo hilo wanasema waliamshwa na milio ya risasi na ndege za kivita zikitua na kuondoka.
Shambulizi hili limetokea siku moja tu baada ya ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani kushambulia kambi moja ya Al shaabab na kuuwa wapiganaji 150.
Alshabab ilipinga idadi hiyo ya wapiganaji ikisema kuwa nambari hizo zimeongezwa chumvi.
Sheikh Abdiasis Abu Musab amenukuliwa akisema kuwa hawakujua ni jeshi lipi lililotekeleza shambulizi hilo ila waliwazima.
''ndege hizo za helikopta zilitua kwenye mto Shabelle na makomando wakaanza kuvizia kambi yetu, hata hivyo tuliweza kuizima ila tulimpoteza mmoja wetu''
''Walikuwa wamebeba roketi na bunduki za M16 mojawepo ya bunduki maarufu sana na jeshi la Marekani.
by Mbwana Ibrahim
Advertisemen
HABARI