Hapa ndipo lilipofikia dili la Aubameyang kwenda Arsenal

Advertisemen
Club ya Arsenal baada ya kumpoteza nyota wake wa kimataifa wa Chile Alex Sanchez aliyeamua kujiunga na Man United ya England, bado dhamira yao ya kumnasa staa wa kimataifa wa Gabon na club ya Borussia Dortmund ya Ujerumani Pierre Emerick-Aubameyang haijafa.
Arsenal leo wameripotiwa na mitandao mikubwa ya habari za michezo duniani kufikia mahala pazuri na Borussia Dortmund, tofauti na ilivyokuwa awali, sasa baada ya kukataliwa kwa ofa zao mbili zilizokuwa zinatajwa kufikia pound milioni 50, ofa yao ya pound milioni 55 imekubaliwa.

Taarifa hizo zimeripotiwa na gazeti la kijerumani linaloamini Kicker lakini likaeleza kuwa Oliver Giroud hawezi kwenda Chelsea kama inavyoripotiwa, kama dili la Aubameyang litakamilika basi ndio atakuwa mchezaji ghali zaidi katika kikosi cha Arsenal baada ya Alexandre Lacazette kusaliwa kwa pound milioni 52.  

by MBWANA IBRAHIM
Advertisemen

Disclaimer: Gambar, artikel ataupun video yang ada di web ini terkadang berasal dari berbagai sumber media lain. Hak Cipta sepenuhnya dipegang oleh sumber tersebut. Jika ada masalah terkait hal ini, Anda dapat menghubungi kami disini.
Related Posts
Disqus Comments